Uhuru, Magufuli waapa kukabiliana vilivyo na wahalifu ▷ Kenya News

– Uhuru na Magufuli waliapa kutumia mbinu za kila aina kukabiliana na wahalifu katika nchi hizi mbili

– Magufuli alisema Mkenya atakayevunja sheria akiwa nchini Tanzania atakabiliwa vilivyo sawa na Mtanzania atakayevunja sheria za Kenya

– Marais hao waliafikiana kwamba amani lazima idumishwe katika nchi hizi mbili

Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli wameapa kukabiliana na wahalifu kwa vyovyote vile.

Akizungumza Jumamosi Julai 6, Magufuli alisema Mtanzania yeyote anayeishi Kenya na apatikane na hatia atakabiliwa vilivyo kisheria.

Habari Nyingine: DP Ruto ajipata taabani huko Migori baada ya vijana kumkemea

Vivyo hivyo, Mkenya anayeishi Tanzania akivunja sheria za nchi hiyo atakabiliwa ipasavyo bila ya huruma.

” Iwapo Mtanzania atavunja sheria za Kenya, atakabiliwa ipasavyo kulingana na sheria ya Kenya, na iwapo Mkenya atavunja sheria ya Tanzania atakabliwa vivyo hivyo,” Alisema Magufuli.

Habari Nyingine: Uhuru Kenyatta amuombea mamake Magufuli alipomtembelea hospitalini

Magufuli aliyasema haya kabla ya kumuaga Uhuru aliyekuwa nchini humo kwa ziara ya siku mbili.

Kwa upande wake, Uhuru alisema nchi hizi mbili zitaimarisha sekta ya kibiashrara na kuhakikisha kwamba amani inadumishwa.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke