Mtangazaji Jacque Maribe ajiuzulu ▷ Kenya News

Mtangazaji Jacque Maribe amejiuzulu kutoka Citizen TV.

Duru za kuaminika zinaarifu kwamba, Maribe alijuzulu Ijumaa, Julai 5.

TUKO.co.ke imebaini kwamba mwanahabari huyo alitaja sababu za kibinafsi katika barua yake ya kujiuzulu.

Maribe na mchumba wake Joseph Irungu maarufu kama Jowie wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Mwanahabari huyo aliachiliwa kwa thamana ya KSh 1 milioni huku Jowie akisalia kizuizini baada ya kukana mashtaka ya kumuua mwanabiashara huyo.

Mfanyikazi mwenzake ambaye hakutaka kutajwa aliinong’onezea TUKO.co.ke kwamba huenda Maribe alijiuzulu kutokana na kesi hiyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko News